sw_2sa_text_reg/17/01.txt

1 line
485 B
Plaintext

\v 1 Kisha Ahithofeli akamwambia Absalomu, "Niruhusu sasa nichague watu elfu kumi na mbili nami nitaondoka na kumfuatia Daudi usiku huu. \v 2 Nitampata kwa ghafla wakati amechoka na dhaifu nami nitamstukiza kwa hofu. Watu waliopamoja naye watakimbia nami nitamshambulia mfalme peke yake. \v 3 Nitawarejesha watu wote kwako kama bibi harusi ajavyo kwa bwana wake, na watu wote watakuwa katika amani chini yako." \v 4 Alichokisema Ahithofeli kikampendeza mfalme na wazee wote wa Israeli.