sw_2sa_text_reg/17/24.txt

1 line
410 B
Plaintext

\v 24 Ndipo Daudi akaja Mahanaimu. Lakini Absalomu yeye akavuka Yordani yeye pamoja na watu wote wa Israeli waliokuwa pamoja naye. \v 25 Absalomu alikuwa amemweka Amasa juu ya jeshi badala ya Yoabu. Naye huyo Amasa alikuwa mwana wa Yetheri Mwishmaeli, aliyekuwa amelala na Abigaili, aliyekuwa binti Nahashi na dada wa Seruya, mamaye Yoabu. \v 26 Kisha Israeli na Absalomu wakapiga kambi katika nchi ya Gileadi.