sw_2sa_text_reg/16/03.txt

1 line
389 B
Plaintext

\v 3 Mfalme akauliza, "Na mjukuu wa bwana wako yuko wapi?" Siba akamjibu mfalme, "Tazama, yeye amesalia Yerusalemu kwa maana alisema, 'Leo nyumba ya Israeli itanirudishia ufalme wa baba yangu." \v 4 Kisha mfalme akamwambia Siba, "Tazama, yote yaliyomilikiwa na Mefiboshethi sasa yatakuwa yako." Siba akajibu, "Nainama kwa unyenyekevu kwako bwana wangu mfalme. Na nipate kibali mbele zako."