sw_2sa_text_reg/12/01.txt

1 line
512 B
Plaintext

\c 12 \v 1 Kisha Yahwe akamtuma Nathani kwa Daudi. Akaja kwake na kusema, "Kulikuwa na watu wawili katika mji. Mmoja alikuwa tajiri na mwingine alikuwa maskini. \v 2 Yule tajiri alikuwa na kundi la ng'ombe na kondoo wengi sana, \v 3 lakini maskini hakuwa na chochote isipokuwa mwanakondoo, aliyekuwa amemnunua na kumlisha na kumlea. Akakua pamoja naye na pamoja na watoto wake. Yule mwanakondoo hata alikula naye na kunywa kutoka katika kikombe chake, naye akalala katika mikono yake na alikuwa kama binti kwake.