sw_2sa_text_reg/04/05.txt

1 line
467 B
Plaintext

\v 5 Hivyo wana wa Rimoni Mbeerothi, Rekabu na Baana, wakasafiri mchana wakati wa jua kali mpaka nyumbani mwa Ishbothethi, yeye alikuwa amepumzika mchana. \v 6 Mwanamke aliyekuwa akililinda lango alisinzia wakati akipepeta ngano, Rekabu na Baana waliingia ndani polepole na wakampita. \v 7 Hivyo walipoingia ndani ya nyumba, walimpiga na kumuua wakati amelala chumbani mwake. Kisha wakakata kichwa chake na wakaondoka nacho, wakasafiri njiani usiku kucha mpaka Araba.