sw_2sa_text_reg/07/18.txt

1 line
403 B
Plaintext

\v 18 Kisha mfalme Daudi akaingia ndani na kuketi mbele ya Yahwe; akasema, "Mimi ni nani, Yahwe Mungu, na familia yangu ni nini hata umenileta hapa nilipo? \v 19 Na hili lilikuwa jambo dogo mbele yako, Bwana Yahwe. Hata ukasema kuhusu familia ya mtumishi wako wakati mkuu ujao, nawe umenionyesha vizazi vijavyo, Bwana Yahwe! \v 20 Mimi Daudi, niseme nini zaidi kwako? Umemjua mtumishi wako, Bwana Yahwe.