sw_2sa_text_reg/07/12.txt

1 line
378 B
Plaintext

\v 12 Siku zako zitakapokwisha na ukalala pamoja na baba zako, nitainua mzao baada yako, atokaye katika mwili wako mwenyewe, nitauimarisha ufalme wake. \v 13 Naye atajenga nyumba kwa jina langu, nami nitakiimarisha kiti chake cha enzi daima. \v 14 Nitakuwa baba kwake, naye atakuwa mwanangu. Atakapotenda dhambi, nitamwadhibu kwa fimbo ya wanadamu na kwa mapigo ya wana wa watu.