sw_2sa_text_reg/23/15.txt

1 line
583 B
Plaintext

\v 15 Daudi alitamani maji na akasema, "Kama ingekuwa mtu mmoja angenipa maji ya kunywa kutoka kisima kilichopo Bethlehemu, kisima kilichopo langoni!" \v 16 Hivyo mashujaa hawa watatu wakapita kati ya jeshi la Wafilisti na kuchota maji katika kisima cha Bethlehemu, kilichopo langoni. Wakachukua maji na kuyaleta kwa Daudi, lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake akayamwaga mbele za Yahwe. \v 17 Kisha akasema, "Iwe mbali nami, Yahwe, kwamba niyanywe haya. Je ninywe damu ya watu waliohatarisha maisha yao?" Hivyo akakataa kuyanywa. Haya ni mambo yaliyofanywa na mashujaa watatu.