sw_2sa_text_reg/17/21.txt

1 line
382 B
Plaintext

\v 21 Ikawa baada yao kuondoka Yonathani na Ahimaasi wakatoka ndani ya kisima. Wakaenda kumtaarifu mfalme Daudi; wakamwambia, "Inuka na uvuke maji haraka kwa maana Ahithofeli ametoa mashauri haya na haya juu yako." \v 22 Kisha Daudi akainuka pamoja na watu wote walikuwa pamoja naye, nao wakauvuka Yordani. Hata ilipofika alfajiri hakuna hata mmoja aliyesalia kwa kutouvuka Yordani.