sw_2sa_text_reg/17/08.txt

1 line
654 B
Plaintext

\v 8 Hushai akaongeza, "Unamjua baba yako na kwamba watu wake ni mashujaa na kwa sasa wanauchungu, ni kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake mwituni. Baba yako ni mtu wa vita; hatalala na jeshi usiku huu. \v 9 Tazama, kwa wakati huu pengine amejificha katika shimo fulani au mahali pengine. Itakuwa kwamba baadhi ya watu wako watakapokuwa wameuawa mwanzoni mwa shambulio hata kila mtu atakayesikia atasema, mauaji yamefanyika kwa askari wanaomfuata Absalomu.' \v 10 Kisha hata askari jasiri zaidi ambao moyo wao ni kama moyo wa simba, wataogopa kwa kuwa Israeli yote inajua kwamba baba yako ni mtu mwenye nguvu na kwamba watu alionao ni wenye nguvu sana.