sw_2sa_text_reg/24/21.txt

1 line
521 B
Plaintext

\v 21 Kisha Arauna akasema, "Kwa nini bwana wangu mfalme amekuja kwangu, mtumishi wake? Daudi akajibu, "Kununua uwanja wako wa kupuria, ili nimjengee Yahwe madhabahu, ili kwamba tauni iondolewe kwa watu." \v 22 Arauna akamwambia Daudi, "Chukua liwe lako, bwana wangu mfalme. Ulifanyie lolote lililojema machoni pako. Tazama, ng'ombe kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na miganda ya kupuria na nira kwa kuni. \v 23 Haya yote bwana wangu mfalme, mimi Arauna nakupa." Kisha akamwambia mfalme, "Yahwe Mungu wako na awe nawe."