\v 10 Ndipo moyo wa Daudi ukamsumbua baada ya kuwahesabu watu. Hivyo akamwambia Yahwe, "Kwa kufanya hivi nimetenda dhambi sana. Sasa, Yahwe, uiondoe hatia ya mtumishi wako, kwani nimetenda kwa upumbavu."