sw_2sa_text_reg/23/20.txt

1 line
371 B
Plaintext

\v 20 Benaya kutoka Kabseeli mwana wa Yehoyada; alikuwa mtu hodari aliyefanya matendo makuu. Aliwauwa wana wawili wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka shimoni na kuuwa simba wakati wa theruji. \v 21 Na alimuua Mmisri aliyekuwa mtu mnene sana. Mmisri alikuwa na mkuki mkononi, lakini Benaya alipigana naye kwa fimbo tu. Aliuchukua mkuki mkononi mwa Mmisri na kisha kumuua nao.