sw_2sa_text_reg/21/07.txt

1 line
591 B
Plaintext

\v 7 Lakini mfalme akamuifadhi Mefiboshethi mwana wa Yonathani mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha Yahwe kati ya Daudi na Yonathani mwana wa Sauli. \v 8 Mfalme akawachukua wana wawili wa Rispa binti Ayia aliomzalia Sauli, hawa wana wawili waliitwa Armoni na Mefiboshethi; na pia Daudi akawachukua wana watano wa Mikali binti Sauli, aliomzalia Adrieli mwana wa Berzilai Mmeholathi. \v 9 Akawaweka katika mikono ya Wagibeoni. Nao wakawatundika juu ya mlima mbele za Bwana, na wote saba wakafa pamoja. Waliuawa katika kipindi cha mavuno, katika siku ya kwanza mwanzoni mwa mavuno ya shayiri.