sw_2sa_text_reg/20/11.txt

1 line
483 B
Plaintext

\v 11 Kisha mmoja wa watu wa Yoabu akasimama kando ya Amasa naye akasema, "Aliye upande wa Yoabu na aliyeupande wa Daudi na amfuate Yoabu." \v 12 Amasa akawa anagalagala katika damu yake katikati ya njia. Mtu yule alipoona kwamba watu wote wamesimama, akambeba Amasa na kumuweka shambani kando ya njia. Akatupa vazi juu yake kwa maana aliona kila mmoja aliyekuja alisimama pale. \v 13 Baada ya Amasa kuondolewa njiani watu wote wakamfuata Yoabu katika kumfuatia Sheba mwana wa Bikri.