sw_2sa_text_reg/20/01.txt

1 line
458 B
Plaintext

\c 20 \v 1 Ikatukia pia kuwa katika eneo lilelile kulikuwa mtu asiye na thamani jina lake Sheba mwana wa Bikri Mbenjamini. Akapiga tarumbeta na kusema, "Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya kila mtu na aende hemani mwake, Israeli!" \v 2 Hivyo watu wote wa Israeli wakamuacha Daudi na kumfuata Sheba mwana wa Bikri. Lakini watu wa Yuda wakamfuata mfalme wao kwa karibu sana, kutoka Yordani njia yote hadi Yerusalemu.