sw_2sa_text_reg/19/07.txt

1 line
473 B
Plaintext

\v 7 Sasa basi, inuka na uende kuongea na askari wako kwa upole, kwani nakuapia kwa Yahwe, ikiwa hutakwenda hakuna mtu hata mmoja atakayesalia nawe usiku huu. Na hii itakuwa vibaya sana kwako kuliko madhara yoyote yaliyowai kukupata tangu ujana wako." \v 8 Hivyo mfalme akainuka na kuketi kati ya lango la mji, watu wote wakaambiwa, "Tazama, mfalme ameketi kati ya lango." Ndipo watu wote wakaja mbele za mfalme. Walakini, Israeli walikuwa wamekimbia kila mtu hemani mwake.