\c 19 \v 1 Yoabu akaambiwa, "Tazama, mfalme analia na kumuomboleza Absalomu." \v 2 Hivyo siku ile ushindi uligeuzwa kuwa maombolezo kwa jeshi lote, kwa maana jeshi likasikia ikisemwa siku hiyo, "Mfalme anaomboleza kwa ajili ya mwanaye."