sw_2sa_text_reg/18/31.txt

1 line
551 B
Plaintext

\v 31 Mara Mkushi akafika na kusema, "Kuna habari njema kwa bwana wangu mfalme kwa kuwa leo Yahwe amekulipia kisasi kwa wale wote walioinuka kinyume chako." \v 32 Ndipo mfalme akamuuliza, "Je huyo kijana Absalomu ni mzima?" Mkushi akajibu, "Adui wa bwana wangu mfalme na wote wainukao kukudhuru na wawe kama huyo kijana." \v 33 Ndipo mfalme alipohuzunishwa sana, naye akaenda chumbani juu ya lango na kulia. Kadili alivyokwenda aliomboleza, mwanangu Absalomu, mwanangu, mwanangu Absalomu! afadhali ningekufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu!"