sw_2sa_text_reg/18/28.txt

1 line
518 B
Plaintext

\v 28 Ndipo Ahimaasi akaita na kumwambia mfalme, "Yote ni mema." Kisha akainama yeye mwenyewe uso wake chini mbele ya mfalme na kusema, Atukuzwe Yahwe Mungu wako, aliyewatoa watu walioinua mkono wao kinyume cha bwana wangu mfalme." \v 29 Hivyo mfalme akauliza, "Je huyo kijana Absalomu hajambo?" Ahimaasi akajibu, "Wakati Yoabu ananituma kwako mfalme, mimi mtumishi wa mfalme, niliona fujo kubwa sana lakini sikutambua ilihusu nini." \v 30 Mfalme akamwambia, "Geuka usimame kando." Hivyo Ahimaasi akageuka na kusimama.