sw_2sa_text_reg/18/24.txt

1 line
373 B
Plaintext

\v 24 Basi Daudi alikuwa amekaa kati ya lango la ndani na lango la nje. Na mlinzi alikuwa juu ya lango ukutani naye akainua macho yake. Alipokuwa akiangalia, akamwona mtu anakaribia huku akikimbia peke yake. \v 25 Mlinzi akaita kwa sauti na kumwambia mfalme. Ndipo mfalme akasema, "Ikiwa yupo peke yake ana habari katika kinywa chake." Mkimbiaji akasogea na kuukaribia mji.