sw_2sa_text_reg/18/06.txt

1 line
297 B
Plaintext

\v 6 Hivyo jeshi likaenda nyikani dhidi ya Israeli; vita ikaenea katika msitu wa Efraimu. \v 7 Jeshi la Israeli likashindwa mbele ya askari wa Daudi; kulikuwa na machinjo makuu kwa watu elfu ishirini siku hiyo. \v 8 Vita ikaenea katika eneo lote na watu wengi wakaangamizwa na msitu kuliko upanga.