sw_2sa_text_reg/18/03.txt

1 line
395 B
Plaintext

\v 3 Lakini watu wakasema, "Wewe usiende vitani, kwani ikiwa tutakimbia hawatatujali sisi, ama nusu yetu wakifa hawatajali. Lakini wewe ni zaidi ya elfu kumi yetu sisi! Kwa hiyo ni afadhali zaidi ukitusaidia ukiwa mjini." \v 4 Hivyo mfalme akawajibu, "Nitafanya lolote lionekanalo jema machoni penu." Mfalme akasimama kati ya lango la mji wakati jeshi lilipoondoka katika mamia na katika maelfu.