sw_2sa_text_reg/17/17.txt

1 line
509 B
Plaintext

\v 17 Yonathani na Ahimaasi walikuwako katika chemichemi za En Rogeli. Hivyo kijakazi mmoja alikuwa akienda na kuwapasha habari waliyopaswa kuifahamu, ili kwamba wasihatarishe maisha yao kwa kuonekana wakiingia mjini. Ujumbe ulipofika ndipo walikuwa wanaenda kumpasha habari mfalme Daudi. \v 18 Lakini kijana mmoja akawaona wakati huo na akamwambia Absalomu. Hivyo Yonathani na Ahimaasi wakaenda kwa haraka na wakaingia katika nyumba ya mtu mmoja huko Bahurimu, aliyekuwa na kisima uani mwake, wakashuka humo.