sw_2sa_text_reg/17/05.txt

1 line
390 B
Plaintext

\v 5 Kisha Absalomu akasema, "Sasa mwiteni pia Hushai Mwarki ili tusikie yeye pia anavyosema." \v 6 Hushai alipofika kwa Absalomu, Absalomu akamweleza kile ambacho Ahithofeli alikuwa amesema na kisha akamwuliza Hushai, "Je tufanye alivyosema Ahithofeli? Ikiwa hapana, tueleze kile unachoshauri." \v 7 Hivyo Hushai akamwambia Absalomu, "Ushauri aliotoa Ahithofeli siyo mzuri kwa wakati huu."