sw_2sa_text_reg/16/20.txt

1 line
308 B
Plaintext

\v 20 Kisha Absalomu akamwambia Ahithofeli, "Tupe shauri lako kuhusu tunachopaswa kufanya." \v 21 Ahithofeli akamwambia Absalomu, "Nenda kwa masuria wa baba yako aliowaacha kutunza kasri, na waisraeli wote watasikia kwamba umekuwa chukizo kwa baba yako. Kisha mikono ya wote walio pamoja nawe itatiwa nguvu."