sw_2sa_text_reg/16/01.txt

1 line
522 B
Plaintext

\c 16 \v 1 Daudi alipokuwa amekwenda kitambo juu ya kilele cha kilima, Siba mtumishi wa Mefiboshethi akaja kumlaki akiwa na punda wawili waliokuwa wamebeba vipande mia mbili vya mikate, vishada mia moja vya mizeituni, vishada mia moja vya tini na mfuko wa ngozi uliojaa mvinyo. \v 2 Mfalme akamuuliza Siba, "Kwa nini umeleta hivi vitu?" Siba akajibu, "punda ni kwa ajili ya familia yako kupanda, mikate na matunda ni kwa ajili ya matumizi ya askari wako, na mvinyo ni kwa ajili ya kunywa kwa yeyote atakayezimia nyikani."