sw_2sa_text_reg/15/32.txt

1 line
436 B
Plaintext

\v 32 Ikawa Daudi alipofika juu njiani mahala Mungu alipokuwa akiabudiwa, Hushai Mwarki akaja kumlaki vazi lake likiwa limeraruliwa na mavumbi kichwani pake. \v 33 Daudi akamwambia, "Ikiwa utaenda nami utakuwa mzigo kwangu. \v 34 Lakini ukirudi mjini na kumwambia Absalomu, 'Nitakuwa mtumishi wa mfalme kama nilivyokuwa mtumishi wa baba yako, ndivyo nitakavyokuwa mtumishi wako,' ndipo utayageuza mashauri ya Ahithofeli kwa ajili yangu.