sw_2sa_text_reg/15/21.txt

1 line
528 B
Plaintext

\v 21 Lakini Itai akamjibu mfalme na kusema, "Kama Yahwe aishivyo na kama bwana wangu mfalme aishivyo, kwa hakika mahali popote bwana wangu mfalme aendako, mtumishi wako pia ndipo atakapokwenda, kwamba ni maisha au kifo." \v 22 Hivyo Daudi akamwambia Itai, haya tangulia uende pamoja nasi." Hivyo Itai Mgiti akaenda pamoja na mfalme, pamoja na watu wake wote na familia zao zote. \v 23 Nchi yote ikalia kwa sauti kama watu walivyokuwa wakivuka Bonde la Kidroni, na pia mfalme naye akivuka. Watu wote wakasafiri kuelekea nyikani.