sw_2sa_text_reg/13/32.txt

1 line
421 B
Plaintext

\v 32 Yehonadabu mwana wa Shama, nduguye Daudi, akajibu na kusema, "Bwana wangu asidhani kuwa vijana wote ambao ni wana wa mfalme wameuawa, kwa maana ni Amnoni pekee ndiye aliyeuawa. Absalomu alilipanga jambo hili tangu siku ile Amnoni alivyomdhulumu Tamari, dada yake. \v 33 Kwa hiyo basi, bwana wangu mfalme asiiweke taarifa hii moyoni, kudhani kwamba wana wote wa mfalme wameuawa, kwani aliyeuawa ni Amnoni peke yake."