sw_2sa_text_reg/13/20.txt

1 line
406 B
Plaintext

\v 20 Absalomu, kaka yake, akamwambia, "Amnoni, kaka yako, amekuwa nawe? Lakini sasa nyamaza, dada yangu. Yeye ni kaka yako. Usiliweke hili moyoni." Hivyo Tamari akakaa peke yake katika nyumba ya Absalomu kaka yake. \v 21 Mfalme Daudi aliposikia haya yote, alikasirika sana. \v 22 Absalomu hakusema chochote kwa Amnoni, kwa maana Absalomu alimchukia kwa kile alichokifanya, kumdhalilisha Tamari, dada yake.