sw_2sa_text_reg/12/26.txt

1 line
348 B
Plaintext

\v 26 Basi Yoabu akapigana na Raba, mji wa kifalme wa watu wa Amoni, naye akaiteka ngome yake. \v 27 Hivyo Yoabu akatuma wajumbe kwa Daudi na kusema, "Nimepigana na Raba, nami nimeshikilia sehemu inayosambaza maji ya mji. \v 28 Kwa hiyo sasa likusanye jeshi lililosalia uhuzingire mji na kuuteka, kwa maana ikiwa nitauteka, utaitwa kwa jina langu."