sw_2sa_text_reg/11/09.txt

1 line
514 B
Plaintext

\v 9 Lakini Uria akalala pamoja na watumishi wa bwana wake katika lango la kasri, wala hakushuka nyumbani kwake. \v 10 Daudi alipoambiwa, "Uria hakushuka nyumbani kwake," akamwambia Uria, Je haukutoka safarini? Kwa nini haukushuka nyumbani kwako?" \v 11 Uria akamjibu Daudi, "Sanduku, na Israeli na Yuda wamo kwenye mahema, na Yoabu na watumishi wa bwana wangu wamepiga hema uwandani. Jinsi gani basi mimi naweza kwenda nyumbani kwangu kula kunywa na kulala na mke wangu? kwa hakika kama uishivyo, sitafanya hivyo.