sw_2sa_text_reg/10/01.txt

1 line
572 B
Plaintext

\c 10 \v 1 Ikawa baadaye mfalme wa watu wa Amoni akafa, na Hanuni mwanaye akawa mfalme mahali pake. \v 2 Daudi akasema, "Nitamtendea wema Hanuni mwana wa Nahashi, kwa kuwa baba yake alinitendea wema." Hivyo Daudi akatuma watumishi wake kumfariji Hanuni kwa habari ya baba yake. Watumishi wake wakaingia katika nchi ya watu wa Amoni. \v 3 Lakini viongozi wa watu wa Amoni wakamwambia Hanuni bwana wao, "Je unadhani kwa hakika Daudi anamheshimu baba yako hata ametuma watu kukutia moyo? Daudi hajawatuma watumishi wake kwako ili kuuangalia mji, kuupeleleza, ili kuuangamiza?