sw_2sa_text_reg/05/08.txt

1 line
427 B
Plaintext

\v 8 Wakati huo Daudi akasema, "Waliowashambulia wayebusi watapaswa kupita katika mfereji wa maji ili wawafikie vilema na vipofu ambao ni adui wa Daudi." Hii ndiyo maana watu husema, "Vipofu na vilema wasiingie katika kasri." \v 9 Hivyo Daudi akaishi ngomeni naye akaiita mji wa Daudi. Akaizungushia ukuta, kuanzia barazani kuelekea ndani. \v 10 Daudi akawa na nguvu sana kwa maana Yahwe, Mungu wa utukufu, alikuwa pamoja naye.