sw_2sa_text_reg/05/03.txt

1 line
406 B
Plaintext

\v 3 Hivyo wazee wote wa Israeli wakaja kwa mfalme huko Hebroni na mfalme Daudi akafanya nao agano mbele ya Yahweh. Wakamtawaza Daudi kuwa mfalme wa Israeli. \v 4 Daudi alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala miaka arobaini. \v 5 Alitawala juu ya Yuda miaka saba na miezi sita huko Hebroni, na huko Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu juu ya Israeli yote na Yuda.