sw_2sa_text_reg/03/28.txt

1 line
492 B
Plaintext

\v 28 Daudi alipolisikia jambo hili akasema, "Mimi na ufalme wangu hatuna hatia mbele za Yahwe daima, kuhusiana na damu ya Abneri mwana wa Neri. \v 29 Hatia ya damu ya Abneri na iwe juu ya Yoabu na nyumba yote ya baba yake. Na asikosekane katika familia ya Yoabu mtu mwenye vidonda, au mwenye ukoma, au kilema atembeaye kwa fimbo au aliyeuawa kwa upanga au mwenye kukosa chakula." \v 30 Hivyo Yoabu na Abishai nduguye wakamuua Abneri, kwa sababu alimuua Asaheli ndugu yao vitani huko Gibeoni.