sw_2sa_text_reg/02/16.txt

1 line
336 B
Plaintext

\v 16 Kila mtu akakamata kichwa cha adui yake na kupiga upanga wake katika ubavu wa adui yake, wakaanguka chini pamoja. Kwa hiyo mahali pale pakaitwa kwa Kiebrania, "Helkath Hazzurim," yaani "konde la upanga," lililopo Gibeoni. \v 17 Vita vikawa vikali sana siku ile na Abneri na watu wa Israeli wakashindwa mbele ya watumishi wa Daudi.