sw_2sa_text_reg/02/04.txt

1 line
311 B
Plaintext

\v 4 Kisha watu wa Yuda wakaja na kumtia Daudi mafuta kuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda. Wakamwambia Daudi, "Watu wa Yabeshi Gileadi wamemzika Sauli." \v 5 Hivyo Daudi akatuma wajumbe kwa wanaume wa Yabeshi Gileadi akawaambia, "Mbarikiwe na Yahwe, kwa kuwa mmeonyesha utiifu huu kwa bwana wenu Sauli mliyemzika.