\v 7 Ikawa mwishoni mwa miaka minne Absalomu akamwambia mfalme, "Tafadhali niruhusu niende ili nitimize nadhili niliyoiweka kwa Yahwe huko Hebroni. \v 8 Kwa maana mtumishi wako aliweka nadhili alipokuwako Geshuri katika Shamu akisema, 'Ikiwa Yahwe kweli atanirejesha Yerusalemu, ndipo nitamwabudu yeye."