\v 6 Hata walipofika katika shinikizo la Nasoni, wale ng'ombe wakakwama, Uza akanyosha mkono wake na kulikumbatia sanduku la Mungu, naye akalishikilia. \v 7 Kisha hasira ya Yahweh ikawaka dhidi ya Uza. Mungu akampiga kwa ajili ya dhambi yake. Uza akafa pale pale kando ya sandaku la Mungu.