\v 9 Kisha mfalme akamwita Siba, mtumishi wa Sauli, na kumwambia, "Yote yaliyo ya Sauli na familia yake nimempa mjukuu wa bwana wako. \v 10 Wewe, wanao, na watumishi wako mtalima mashamba kwa ajili yake nanyi mtavuna mazao ili kwamba mjukuu wa bwana wako apate chakula. Kwa maana Mefiboshethi, mjukuu wa bwana wako, atakula katika meza yangu daima." Basi Siba alikuwa na wana kumi na watano na watumishi ishirini.