\v 15 Daudi akatawala juu ya Israeli yote, naye akatenda kwa haki na usawa kwa watu wote. \v 16 Yoabu mwana wa Seruya alikuwa mkuu wa jeshi, na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mwenye kuandika taarifa. \v 17 Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani, na Seraya alikuwa mwandishi. \v 18 Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi, na wana wa Daudi walikuwa washauri wa mfalme.