\v 7 Daudi akamwambia, "Usiogope, maana hakika nitakufadhiri kwa ajili ya Yonathani baba yako, nami nitakurudishia ardhi yote ya Sauli babu yako, nawe utakula katika meza yangu daima." \v 8 Mefiboshethi akainama na kusema, "Mtumishi wako ni nani, hata ukamwangalia kwa fadhiri mbwa mfu kama nilivyo?"