sw_2co_text_ulb/04/01.txt

1 line
304 B
Plaintext

\v 1 Kwa hiyo, kwa sababu tuna huduma hii, na kama ambavyo tumeipokea rehema, hatukati tamaa. \v 2 Badala yake, tumekataa njia zote za aibu na zilizofichika. Hatuishi kwa hila, na hatulitumii vibaya neno la Mungu. Kwa kuwasilisha iliyo kweli, tunajionyesha wenyewe kwa dhamiri ya kila mtu mbele ya Mungu.