sw_2ch_text_reg/33/07.txt

1 line
694 B
Plaintext

\v 7 Ile sanamu ya Maashera aliyokuwa amefanya, akaiweka katika nyumba ya Mungu. Ni kuhusu nyumba hii ambayo Mungu alikuwa amesema kwa Daudi na Suleimani mwanaye; alikuwa amesema, "Ni katika nyumba hii na katika Yerusalemu, ambao nimeuchangua kutoka makabila yote ya Israeli, kwamba nitaliweka jina langu milele. \v 8 Sitawaondoa tena watu wa Israeli katika nchi hii ambayo niliitoa kwa babu zao, ikiwa tu watakuwa makini katika kuyashika yote niliyowaamuru, kuzishika sheria zangu, amri zangu, na sheria zangu nilizowapa kupitia Musa." \v 9 Manase akawaongoza Yuda na wakaaji wa Yerusalemu hata kufanya uovu zaidi kuliko hata watu wa mataifa ambao Yahwe alikuwa amewateketeza mbele za Israeli.