sw_2ch_text_reg/06/28.txt

1 line
695 B
Plaintext

\v 28 Kama kuna njaa katika nchi, au kama kuna ugonjwa, tauni au ukungu, nzige au viwavijeshi, au kama adui wake wameyavamia malango ya mji katika nchi yao, au kwamba kuna pigo lolote au ugonjwa— \v 29 na ikiwa sala na maombi yamefanywa na mtu au watu wako wote Israel—kila mmoja akilijua pigo na huzuni katika moyo wake akinyosha mikono yake kuelekea hekalu hili. \v 30 Basi sikiliza mbinguni, sehemu ambayo unaishi; samehe, na umlipe kila mtu kwa njia zake zote; uhaujua moyo wake, kwa sababu wewe na ni wewe pekee unaijua mioyo ya wanadamu. \v 31 Fanya hivyo ili kwamba wakuogope wewe, ili waweze kutembea katika katika njia zako siku zote ambazo wataishi katika nchi uliyowapa baba zetu.