1 line
443 B
Plaintext
1 line
443 B
Plaintext
\v 19 Kisha Uzia akakasirika. Alikuwa ameshikilia chetezo mkononi kwa ajili ya kufukiza uvumba. Wakati alipowaghadhabikia makuhani, ukoma ukatokea juu ya uso wake mbele ya makuhani katika nyumba ya Yahwe, pembeni mwa madhabahu ya uvumba. \v 20 Azaria kuhani mkuu na makuhani wote wakamwanagalia, na, tazama, alikuwa amepatwa ukoma juu ya uso wake. Walimwondoa pale haraka. Kwa hakika, aliharakisha kwenda nje, kwa maana Yahwe alikuwa amempiga. |