sw_2ch_text_reg/10/03.txt

1 line
397 B
Plaintext

\v 3 Kwa hiyo wakatuma na kumuita yeye, na Yeroboamu na Israeli wote wakaja; wakamwambia Rehoboamu na kusema, \v 4 "Baba yako aliifanya nira yetu ngumu. Kwa hiyo sasa, ifanye kazi ngumu ya baba yako kuwa rahisi, na ifanye nyepesi nira yako ambayo baba yako aliiweka juu yetu, na sisi tutakutumikia wewe." \v 5 Rehoboamu akawaambia, "Njoni kwangu tena baada ya siku tatu." Kwa hiyo watu wakaondoka.