sw_2ch_text_reg/03/01.txt

1 line
509 B
Plaintext

\c 3 \v 1 Kisha Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya Yahwe katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, ambako Yahwe alimtokea Daudi baba yake. Aliandaa sehemu ambayo Daudi aliikusudia, katika sakafu ya kupuria ya Arauna Myebusi. \v 2 Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili, katika mwaka wa nne wa utawala wake. \v 3 Sasa hivi ndinyo vipimo vya ule msingi ambao Sulemani alijenga kwa ajili ya nyumba ya Mungu. Akitumia mtindo wa vipimo vya zamani, urefu ulikuwa mikono sitini, na upana ulikuwa mikono ishirini.